Wafanyabiashara na wadau wilayani Tarime wanufaika na elimu ya GePG toka TRA


Na Timoty Itembe Mara.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoani Mara jana  imetambulisha mfumo mpya Gate elektronikali la ukusanyaji kodi na madhuhuri ya Serikali (GePG) kwa wafanyabiashara na Wadau  wilaya Tarime.

Semina hiyo ilifanyikia katika ukumbi wa Hoteli ya Moroni Gardeni uliopo Njia ya Nyamwaga Road ikiwa na lengo la kukusanya Kodi ya serikali na kuinua uchumi wa Taifa

Akizungumza Afisa Elimu na huduma kwa mlipa Kodi TRA Mkoani Mara,Zake Wilbard alisema kuwa mfumo huo umeboreshwa tofauti na mifumo iliyokuwepo ya ukusanyaji kodi na madhuhuri ya Serikali hapo nyuma na kuwa mfumo huo umeanza kutumika mwezi huu wa Saba mwaka 2020.



“Mufumu utapunguza makosa mbali mbali ya mlipa kodi kwa kutumia Mwaamala utakaokuwa umetumiwa na mlipa kodi na kupunguza ujanja ujanja kupitia namba ya mlipa kodi TIN Namba iliyosajiliwa ambayo imeboreshwa”alisema Wilbard.



Afisa huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wafanyabiashara na Wadau kwa ujumla kujiunga na mfumo huu ambao tayari makampuni mengine kama vile TANESCO wanautumia.


Kwa upande wake Magesa Simija mjasilia mali karakana ya Aliminium alitumia nafasi hiyo kupongeza  TRA na kuwataka pindi wanapoenda kutoa elimu watumie viongozi wa serikali wa eneo husika kama vile mkurugenzi wa halmashauri ama mkuu wa wilaya kwa lengo la kuwahimiza wafanyabiashara na wadau kuhudhuria mafunzao ya semina itakayokuwa imeandaliwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia