Zoezi la kutafuta miili ya watu kwenye mgodi wa madini nchini Mynamar lasitishwa


Zoezi la kutafuta miili ya watu waliokwama kwenye mgodi wa madini ya Jade nchini Mynamar limesitishwa kufuatia mvua kumbwa zinazoendelea kunyesha na hivyo kuzuia kupatikana kwa watu waliokwama na ambao huenda tayari wamepoteza maisha kutokana na tope linalozidi kuporomoka na kufanya zoezi hilo kuwa gumu.

Mpaka sasa miili ya watu 113 pekeendio imekwishapatikana ambapo Polisi wa eneo hilo wamesema, wachimbaji hao walikaidi onyo la kutofanya kazi katika migodi hiyo wakati wa mvua.

Msemaji wa kikosi cha uokoaji nchini Myanmar Than Win Aung, amesema vifo vingi zaidi vingeripotiwa endapo wasingechukua hatua ya kuwaonya wachimbaji waliokuwa katika mgodi uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema, Mgodi huo uliporomoka na kuwafunika wachimbaji hao kwa tope zito baada ya mvua kubwa kunyesha karibu na mpaka wa China katika jimbo la Kachin.