Mawakili wa Hong Kong wasema kuahirishwa uchaguzi ni kinyume cha sheria


Chama cha mawakili cha Hong Kong kimesema hatua ya serikali ya mji huo ya kuahirisha uchaguzi wa bunge kwa mwaka mmoja baada ya ongezeka la maambukizi ya virusi vya corona ni kinyume cha sheria.

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam Ijumaa iliyopita aliahirisha uchaguzi huo akitaja hatari za kiafya ila akasema kulikuwepo na masuala ya kisiasa ndani yake.

 Uchaguzi huo ungekuwa wa kwanza rasmi katika koloni hilo la zamani la Uingereza tangu China ilipoweka sheria ya usalama kukabiliana na kile China inachokiita kujitenga, ugaidi na ushirikiano na uingiliaji kutoka nje, sheria ambayo ukiukaji wake unaadhibiwa kwa kifungo cha maisha.

Sheria za uchaguzi Hong Kong zinakubali kuahirisha kwa uchaguzi kwa siku kumi na nne ila sheria ya tangu enzi za ukoloni inaipa serikali nguvu kubwa iwapo kuna kitisho kwa usalama wa umma
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia