Salim Turky kuzikwa leo Fuoni mkoa wa Mjini Magharibi

Na THABIT MADAI, ZANZIBAR.

ALIYEKUWA mgombea Ubunge wa jimbo la Mpendae kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Salim Turky, ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo Sep 15, 2020, atazikwa leo Saa 10:00 Jioni huko Fuoni Kijito Upele mkoa wa Mjini Magharibi.

Salim Turky alikua ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae miaka mitano iliyopita na pia alikua mgombea ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, ambapo imeelezwa kuwa na hata juzi katika ufunguzi wa kampeni za CCM Zanzibar uliofanyika viwanja vya Demokrasia Mjini Unguja.

Katika uzinduzi huo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, alimpa fursa ya kujinadi na kuomba kura kwa wanachama wa CCM wa Jimbo la Mpendae ambao waliohudhuria. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mpendae na maiti itaswaliwa katika Masjid Muhammad (Msikiti wa Othman Maalim), uliopo Mchina Mwanzo na marehemu atazikwa Fuoni Kijito Upele Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa ilitolewa na mtoto wake Toufiq Salim Tyrky kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ilisema ni kweli taarifa zinazotolewa za kifo cha Mgombea huyo ambaye ni baba yake mzazi ni za kweli.

"Assalam aleykum nawapa taarifa kuwa nimefiwa na baba yangu mzazi Mr.Salim Hassan Abdullah Turky usiku wa kuamkia leo inna lilahi wainna illaihi rajiuun,"alisema

Katika taarifa hiyo ilisema ratiba mazishi ni jana saa 10 jioni,Fuoni Kijitoupele na si Fumba kama wengine walivyotangaza.

Mbali na kuwa mwanasiasa pia Turky alikuwa mfanyabiashara mkubwa visiwani Zanzibar alizaliwa February 11 mwaka 1963 na hadi mauti yanamfika alikuwa Mwenyekiti wa kampuni 12 ya Turky.

Akizungumzia kifo hicho Katibu wa jimbo la Mpendae wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM), Haji Ali Mussa ambapo alisema akiwa kama mtu ambaye alikuwa anafanyanaye kazi kwa karibu katika kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa ya kifo chake.

Katibu huyo alisema kwa upande wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na UVCCM wamepokea kwa masikitiko taarifa hiyo yha kifo chake ambacho kimetokea ghalfa na kwamba mgombea alikuwa anawajali wananchi wa jimbo la Mpendae.

Katika maelezo yake alisema mgombea alikuwa ni mtu mwenye maono ambapo alikuwa anafikiria kabla ya kutenda na kwamba alikuwa mtu mwenye kujikosoa kabla ya kukosolewa.

"Alikuwa mtu ambaye anawaomba radhii wananchi kwa mfano alionyesha kuwa yeye ni mtu ambaye anajikosoa juzi alikuwa na kikao cha mkakati kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu katika jimbo la Mpendae na wanachama lakini kuna maneno aliyatoa huku akiwaomba radhii wanachama waliohudhuria kikao hicho,"alisema

Katibu huyo alisema Mgombea huyo aliwawezesha kiuchumi vijana wa jimbo hilo na kwamba vijana wameondokewa na mtu ambaye alikuwa ni msaada mkubwa kwao.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia