Oct 20, 2020

Mfalme Salman ateua viongozi wapya wa baraza la ushauri na bunge la Saudi Arabia


Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulazizi, amefanya uteuzi mpya wa viongozi wa baraza la ushauri na wahudumu wengine wa ngazi za juu wenye majukumu mbalimbali nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Saudi Arabia SPA, iliarifiwa kuwa mfalme Salman aliteua baraza la ushauri linalojumuisha wanachama 150 chini ya usimamizi wa Sheikh Abdullah Al al-Sheikh ili kuhudumu kwa miaka 4.

Wanachama wa baraza la ushauri huteuliwa na mfalme na kisha maamuzi yanayochukuliwa na bunge la Saudi Arabia huhitaji kudhinishwa na mfalme.

Miongoni mwa viongozi wengine walioteuliwa na mfalme Salman chini ya ungozi wa Mufti wa nchi Sheikh Abdulaziz Al al-Sheikh, ni wanachama 20 wasomi wa viwango vya juu, Katibu mkuu wa mahakama ya kifalme Sheikh Gayhab al-Gayhab pamoja na mwenyekiti wa mahakam kuu Sheikh Khalid bin Abdullah bin Mohammad al-Lahidan.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger