Rais wa Urusi Vladimir Putin amependekeza kurefushwa kwa mkataba wa Urusi na Marekani wa kudhibiti silaha unaofahamika kama New START, kwa mwaka mmoja bila masharti yoyote.
Mkataba huo ulikuwa unafikia mwisho mwezi Februari. Mkataba huo uliotiwa saini mwaka 2010 unaweka kiwango cha idadi ya vichwa vya nyuklia, makombora na mabomu kinachoweza kumilikiwa na Marekani na Urusi.
Iwapo mkataba huo hautaongezwa vikwazo vyote vilivyoko vya Marekani na Urusi katika suala hilo la zana za nyuklia vitasita, na huenda jambo hilo likachochea vita baridi vya kuwania silaha na mivutano kati ya Urusi na Marekani.
Putin anasema mkataba huo umefanikiwa miaka yote hiyo na itakuwa ni huzuni mno iwapo hautaendelea.
