Serikali kuu ya Uhispania yatangaza hatua mpya kukabiliana na COVID-19

Serikali kuu nchini Uhispania leo imetangaza hatua mpya za kukabiliana na virusi vya corona zinazojumuisha marufuku ya shughuli za kawaida kwenye mji mkuu Madrid, licha ya upinzani kutoka serikali ya jimbo. 

Amri hiyo iliyochapishwa leo katika gazeti la serikali na waziri wa afya wa Uhispania Salvador Illa inailenga miji mikubwa iliyo na idadi inayoongezeka ya maambukizi ya COVID-19 na kiwango fulani cha wagonjwa mahututi. 

Vizuizi hivyo vipya vinavyohusisha hatua kali za kujitenga na marufuku ya matembezi vitaanza kufanya kazi kwenye mji mkuu Madrid na miji mingine tisa iliyo katika jimbo la Community Madrid. 

Hata hivyo tayari kiongozi wa jimbo uliko mji mkuu, Madrid, amesema hawatatekeleza amri hiyo ya serikali kuu na wananuwia kuipinga kwenye mahakama ya juu ya Uhispania.


 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia