Bajeti ya EU na mpango wa uokozi uchumi bado kizungumkuti

 


Afisa mkuu anayehusika na uchumi katika Tume ya Umoja wa Ulaya Paolo Gentiloni, amezihimiza nchi wanachama kuunga mkono bajeti ya euro bilioni 1.8 na mpango wa uokozi wa janga la virusi vya corona, baada ya Hungary na Poland kuzuia uidhinishwaji wake. 

Gentiloni amesema nchi wanachama zinapaswa kuonyesha dhamira ya uwajibikaji kwa raia wao katika wakati huu mgumu. Siku ya Jumatatu Hungary na Poland zilizuia uidhinishwaji wa mpango wa uokozi na bajeti ya mwaka 2021-2027 kuhusiana na mvutano juu ya utawala wa sheria. 

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema Umoja wa Ulaya unataka kuhusisha masuala hayo na nchi kuheshimu utawala wa sheria, ili kuilazimisha nchi yake kukubali wahamiaji. 

Ujerumani inayoshikilia urais wa kupokezana wa Umoja huo, imeapa kuyashawishi mataifa hayo mawili kuondoa zuio hilo katika mkutano wa kilele utakaofanyika kesho.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia