China yapinga vikwazo vya Marekani dhidi ya raia wake wanne

 


China imesema kuwa vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya raia wake wanne, kuhusiana na hatua za China jijini Hong Kong, ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na inaingilia kati maswala ya jiji hilo. 

Marekani iliwawekea vikwazo raia hao wa China hapo jana Jumatatu kwa kuhusika na ukandamizaji wa demokrasia katika mji wa Hong Kong. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin ameihimiza Marekani kuondoa vikwazo hivyo mara moja, ili kuepuka kuvurugika zaidi uhusiano kati ya mataiafa hayo mawili.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items