Kisa upandaji bei ya saruji Waziri mkuu atoa agizo kwa wakuu wa mikoa


Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha hadi kufikia tarehe 20, Novemba, 2020 wanafahamu ni kwanini bei ya saruji imepanda kutoka bei ya kawaida kwa kutembelea viwanda na mawakala wa saruji  wakati serikali haijapandisha kodi.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo akiwa Ikulu ya Rais Chamwino mara baada ya kuapishwa, ambapo amemuhakikishia Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa ameshaanza  kulishughulikia suala la upandaji wa bei ya saruji.

“Wako wenzetu wachache wameanza kujisahau wakidhani serikali iko kwenye uchaguzi na tumeona kumeibuka upandaji bei wa saruji kwa gharama kubwa sana ambazo hazikubaliki na hakuna sababu ya msingi , serikali yetu imefanya mambo makubwa sana hatutarajii saruji kuwa na bei hiyo ambayo tumeiona” amesema Waziri Majaliwa 

Aidha,kwa kukazia suala hilo, Mh. Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa kote nchini,kutembelea viwanda na mawakala wanaozalisha na kuuza saruji,“Niwaagize ma RC mpaka tarehe 20, asubuhi, kila mmoja aende kwenye kiwanda na mawakala wa saruji waangalie ni kwanini bei ya saruji imepanda kutoka bei ya kawaida na ongezeko la zaida ya Sh. 3000, hadi 4000 wakati serikali haijaongeza kodi”

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia