Shirika la Afya Duniani WHO limekaribisha juhudi za kuliongezea nguvu shirika hilo lililo na makao yake mjini Geneva, Uswisi, kupitia mabadiliko na limesema pia linatazamia kufanya kazi kwa karibu na rais mteule wa Marekani Joe Biden.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ufadhili wa shirika hilo unastahili kuwa unaotabirika.
Rais wa Marekani Donald Trump alisimamisha ufadhili kwa shirika hilo na alianzisha mchakato utakaoshuhudia Marekani kujiondoa kutoka kwenye shirika hilo la afya mnamo mwezi Julai, jambo lililolaaniwa kote duniani wakati ambapo kuna janga la virusi vya corona linaloendelea kuitikisa dunia.
Biden lakini amesema katika siku yake ya kwanza afisini atautengua uamuzi huo wa Trump na kuirudisha Marekani kuwa mwanachama wa WHO.
