Waanzilishi wa chanjo dhidi ya Corona waalikwa na UN

Volkan Bozkır, Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 75 wa Umoja wa Mataifa (UN), amewakaribisha Profesa Daktari Uğur Şahin na Daktari Özlem Türeci, waanzilishi wa kampuni ya bioteknolojia ya Ujerumani BioNTech, ambayo imetengeneza chanjo dhidi ya corona.

Mkutano huo unatarajia kufanyika mnamo tarehe 3-4 Desemba.

Bozkır alisema kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba alikutana na wanasayansi wa Uturuki Şahin na Türeci kupitia mkutano wa video na "anawapongeza kwa dhati" kwa mafanikio yao ambayo yanatoa matumaini kwa ulimwengu wote.

Volkan Bozkır, aliendelea kwa kusema,

"Walikubali mwaliko wangu kama spika wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , ambao nitasimamia Desemba 3-4."

Ilitangazwa kuwa chanjo ambayo BioNTech ilikuwa ikitengeneza dhidi ya Covid-19 ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 90 dhidi ya virusi.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items