Kamanda wa waasi Uganda Ongwen akutwa na hatia ya uhalifu wa kivita

 


Aliyekuwa kamanda wa waasi wa Lords Resistance Army nchini Uganda - LRA Dominic Ongwen amehukumiwa kwa makosa ya uhalifu, ukiwemo ubakaji, utumwa wa ngono, utekaji nyara watoto, mateso na mauaji, ikiwemo mauaji ya watoto wadogo. 


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC imemkuta Ongwen na hatia ya makosa 61 kati ya 70 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu. 


Akitangaza hukumu hiyo, Jaji Bertram Schmitt alisema Ongwen, mwenye umri wa miaka 46, ambaye aliingizwa katika uasi wa LRA akiwa kijana mdogo, alifanya uhalifu huo kwa hiari yake kati ya mwaka wa 2002 na 2004. 


Na kwa mara ya kwanza kisheria, Ongwen pia amehukumiwa kwa uhalifu wa mimba za kulazimishwa kutokana na maovu yaliyofanywa dhidi ya wanawake saba. Adhabu ya hukumu hiyo itatangazwa baadae.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi