Kiwanda kilichofanya kazi miezi 9 na kusimama,kuanza kazi tena kuanzia June


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Chama kikuu cha ushirika mkoani Njombe (NJORECU) kinatarajia kuanza upya uchakataji wa unga wa mahindi kupitia kiwanda kinachomilikiwa na Chama hicho kilichosimama mwaka 2019 ikiwa ni miezi tisa baadaye mara baada ya kufunguliwa na kuanza kufanya kazi mwaka 2018.

Meneja mkuu wa NORECU mkoa wa Njombe Samuel Mlumba,amebainisha hayo katika mkutano na wanachama uliofanyika mjini Njombe,huku akibainisha kuwa zipo sababu mbali mbali ikiwemo changamoto za uongozi zilizosababisha kiwanda hicho kufanya kazi kwa muda mfupi na kutokana kuondoshwa kwa changamoto hizo hakuna sababu itakayozuia kiwanda hicho cha uchakataji wa Sembe kuanza kufanya kazi.

Mlumba amesema Kiwanda  kilichopo mjini Njombe  kilichosimama March 2019 huku kikiwa kimefanya kazi miezi 9 tangu kilipoanza kufanya kazi June 2018 kinatarajiwa kuanza uzalishaji kuanzia June mpaka March mwaka wa fedha wa 2022

“Sababu zilizopelekea kufanya kazi kwa miezi 9 safari hile sasa hivi hazipo,kwasababu zilikuwa ni changamoto za kiutumishi na usimamizi wa kiwanda hicho”alisema Mlumba

Aliongeza “Tupo kwenye mkakati wa kutafuta wataalamu waweze kututengenezea mpango biashara kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata Sembe”aliongeza Mlumba

Nestory Betram ni kaimu mhasibu mkuu wa NJORECU,amesema kabla ya kufika mwaka wa fedha wanatarajia kununua tani za mahindi 1199.7 zenye tahamani ya shilingi milioni 600 kutoka kwenye AMCOS mbali mbali.

Benedict Mwageni ni Mwenyekiti wa bodi ya mpito wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe,ametoa wito kwa wakulima walioko kwenye AMCOS kujiandaa kunufaika kwa kuwa kiwanda hicho kinaenda kuongeza thamani ya mazao.

“Soko la kwanza la mahindi la wana Njombe liwe ni Chama kikuu cha ushirika, kiwanda chetu kitakapoanza kufanya kazi,tunatarajia kila siku kuchakata Mahindi tani zisizokuwa pungufu ya 15 kwa hiyo kwa mwaka tutakuwa na kilo 4500”alisema Benedict Mwageni

Romanus Lugome na Mariana Chaula ni miongoni wa viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) mkoani Njombe wameshukuru uongozi wa Chama Kikuu kuona namna ya kufufua matumaini ya muda mrefu ya Chama kundeleza miradi yao ikiwemo kiwanda hicho kitakachokuwa na msaada kwa wakulima wa Mahindi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items