Serikali yatolea Ufafanuzi kufungwa kwa kiwanda cha kuchinja Punda Shinyanga


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeitaka kampuni ya Fang Hua Investment ya Ibadakuli Wilaya ya Shinyanga iliyokuwa ikijihusisha na uchinjaji wa punda na kufutiwa usajili wake Septemba 2020, imetakiwa kufuata taratibu upya za usajili wa kufungua  kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano Wizara ya Mifugo na Uvuvi inasema kumeanza kuibuka kwa taharuki kwa wafanyabiashara wa punda baada ya kiwanda hicho kufungwa, huku Wizara wakiwataka wamiliki wa kiwanda hicho kutoa taarifa sahihi kwa wafanyabiashara hao.

Taarifa hiyo imesema tangu Kampuni hiyo kupoteza uhalali wa usajili wake haijatekeleza ushauri uliotolewa na  kituo cha uwekezaji TIC wa kuwasilisha maombi upya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya leseni.

“kwa siku za hivi karibuni yamejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wakionyesha hisia zao kwamba Wizara ya Mifugo na Uvuvi inakwamisha leseni ya Kampuni hii ya uchinjaji, ni vyema Umma ukafahamu hoja hiyo si kweli na kwamba kampuni yenyewe ndio haijaona haja ya kutekeleza ushauri waliopewa”.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia