Zaidi ya waandamanaji 1,400 wakamatwa baada ya Navalny kuhukumiwa jela

 


Maafisa wa usalama nchini Urusi, wamewakamata zaidi ya waandamanaji 1,400 wakati wa maandamano ya kumuunga mkono mkosoaji wa serikali ya nchi hiyo, Alexei Navalny.

Kundi la kutetea haki za binadamu, OVD-Info, limesema hayo leo, siku moja baada ya Navalny kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka miwili jela.Uamuzi wa kumfunga jela Navalny umeshutumiwa na jumuiya ya kimataifa.

 Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya zikitaka aachiliwe huru mara moja, huku serikali ya Urusi ikisema nchi za Magharibi zinaingilia masuala yake ya ndani.

Mawakili wanaomwakilisha kiongozi huyo wa upinzani wamesema watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.Navalny alihukumiwa baada ya kukutikana na hatia ya kukiuka masharti ya kesi dhidi yake iliyokuwa imesimamishwa kwa muda.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia