Idadi kubwa ya watu wapoteza maisha baada ya kushambuliwa katika soko la mkoa wa Tigray nchini Ethiopia

Idadi kubwa ya watu walipoteza maisha kwenye shambulizi la angani lililotokea katika soko la mkoa wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Ilibainishwa kuwa baada ya shambulizi hilo lililolenga eneo la Togoga mkoa wa Tigray kutekelezwa, wafanyikazi wa afya walizuiwa kwenda katika mkoa huo na vikosi vya usalama.

Mashuhuda wa tukio walisema kuwa watu wengi walifariki katika shambulizi la angani, na majeruhi walipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Serikali bado haijatoa maelezo zaidi juu ya shambulizi hilo la angani.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia