Sep 16, 2021

Kocha wa Manchester United afafanua kuhusu mabadiriko

  Muungwana Blog 3       Sep 16, 2021


OLE Gunnar Solskjaer Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa hakuwa na chaguo la kufanya na kuamua kuwatoa wachezaji wake Cristiano Ronaldo na Bruno Fernandes wakati timu hiyo ikichapwa mabao 2-1 dhidi ya Young Boys kwa kuwa alikuwa anawalinda wachezaji wake.


Ilikuwa ni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati ubao ukisoma Yaoung Boys 1-1  United kocha aliamua kufanya mabadiliko kwa kumtoa Ronaldo ambaye alitupia bao mapema kipindi cha kwanza.


Maamuzi hayo yanatajwa kuwakasirisha mashabiki wengu huku ikiwa ni faida kwa Young Boys waliamua kufunguka na kushinda mchezo huo ambao United walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda ndani ya dakika 90.


Solskjaer amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wamekimbia kiasi cha kutosha na hawakuwa sawa jambo ambalo aliona ni vyema awape mapumziko na kupitia makosa wamejifunza.


Pia mipango inatajwa kuharibika baada ya nyota wao Aaron Wan-Bissaka kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa kwa moja huku Solskjaer akiwa bado hajaelewa sababu ya kadi ile akiamini ilikuwa ni mbinu ya kiufundi.

 

logoblog

Thanks for reading Kocha wa Manchester United afafanua kuhusu mabadiriko

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment