Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kumeweka ulazima wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 na kwamba utekelezaji wa hatua hiyo utaanza Januari.
Ufafanuzi wa mpango huo utatolewa Desemba na kwamba
hatua hiyo itakifanya chuo kikubwa kuwa cha kwanza kuweka masharti ya
chanjo ili mtu aweze kuingia katika maeneo yake.
Afrika Kusini hivi
karibuni ilizindua cheti cha chanjo cha kieletroniki na kwa sasa kipo
katika mjadala kama matumizi yake yawe ya lazima katika baadhi ya maeneo
au la.
Taifa hilo ambalo limeathiriwa vibaya zaidi na virusi vya corona
barani Afrika, limeanza taratibu kutoa chanjo kwa raia wake huku
likikabiliana na hali ya kusitasita.
0 Comments