Korea Kusini yazindua roketi yake ya kwanza

Korea Kusini imezindua roketi yake ya kwanza kutengezwa nyumbani, kupiga hatua katika harakati za nchi katika sayansi za anga za mbali

Roketi hiyo ya Korea, inalojulikana kama Nuri, liliondoka Goheung, karibu 500km (maili 310) kusini mwa Seoul.

Rais Moon Jae-in amesema gari hilo limekamilisha mpango mzima wa safari safari lakini ilifeli kuweka kielelezo cha satelliteyake kwenye mzunguko wa dunia.

Uzinduzi kama huo ni muhimu katika mpago wa anaganilakini huenda ikawa na vifaa vya kijeshi.

Korea Kusini inakimbizana na Korea Kaskazini katika uundaji silaha, nchi zote mbili zikijaribu silaha zao mpya hivi karibuni. Kaskazi ilifikisha satellite yake katika mzunguko 2012.

Nuri iligharimu Korea Kusini karibu dola blioni 1.62 kutengeza. Roketi hiyo yenye uzani wa tani 200 na urefu wa mita 47.2, ina injini sita za mafuta.

Katika maoni yake, Rais Moon alikiri uzinduzi huo haukufikia malengo yao, lakini akaongeza: "Sio muda mrefu kabla ya kuweza kuizindua kikamilifu katika njia inayolengwa," shirika la habari la Reuters liliripoti.

Korea Kusini inapanga kufanya majaribio mengine manne ya chombo cha Nuri hadi 2027 ili kujiimarisha, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Anga ya Korea (KARI) ambayo inasimamia uzinduzi huo.

 

Post a Comment

0 Comments