Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana tena Brussels baada ya mwaka na nusu


Mawaziri wa ulinzi wa kutoka mataifa 30 wanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO wanakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya mwaka mmoja na nusu, kwenye makao makuu ya muungano huo mjini Brussels
 
 Mada za kujadiliwa katika mkutano huo ni ujenzi zaidi wa uwezo wa jumuiya hiyo kuzuwia hujuma na kujilinda, pamoja na juhudi zinazoendelea za kuwarudisha nyumbani wafanyakazi wa jumuiya hiyo waliosalia nchini Afghanistan.
 
 Zaidi ya hayo, mkutano huo utajadili namna ya kuendeleza mipango ya kuwekeza katika teknolojia zinazoinukia. 
 
Kwa muktadha wa kutimiza lengo hilo, mfuko wa ubunifu wenye thamani ya takribani Euro bilioni moja unapangwa kuanzishwa. Mkutano huo hata hivyo umegubikwa na mzozo mpya kati ya jumuiya hiyo na Urusi.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia