Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Iran yaanza kusikiliza kesi ya kudunguliwa kwa ndege ya Ukraine


Mahakama ya kijeshi ya Iran imeanza kusikiliza kesi ya kudunguliwa kwa ndege ya abiria ya Ukraine mnamo mwaka 2000 iliyosababísha vifo vya watu 176. Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa wanajeshi kumi wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo walikuwepo mahakamani. 


Familia za wahanga na mawakili wao pia walihudhuria kikao cha kesi hiyo, wakiwakilisha malalamiko 103 ya kisheria juu ya kudunguliwa kwa ndege ya abiria ya Ukraine nambari PS752. 


Ripoti ya shirika la habari la IRNA imeongeza kuwa jaji ambaye hakutajwa jina lake alisema anatumai mahakama hiyo itatoa hukumu haraka na sahihi kwa kuzingatia utaratibu wenye kufuata haki na sheria. Hii ni mara ya kwanza kwa kesi hiyo kusikilizwa tangu ndege hiyo ilipoanguka yapata 22 iliyopita.

Post a Comment

0 Comments