Aliyekuwa mkuu wa majeshi mwenye ushawishi mkubwa na aliyetwaa madaraka kwa nguvu mnamo mwaka 1979 kupitia mapinduzi nchini Korea Kusini, Chun Doo-Ghwan, amefariki dunia.
Chun aliyeyazima maandamano ya wanaopigania demokrasia nchini humo kabla ya kupelekwa jela kwa madhambi aliyoyafanya alipokuwa madarakani, amefariki leo akiwa na umri wa miaka 90.
Chun aliyekuwa akiugua hivi karibuni maradhi ya kupoteza kumbukumbu pamoja na saratani ya damu amekufa baada ya kupata mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake mjini Seoul, kwa mujibu wa polisi na maafisa wa huduma za dharura.