Wanafunzi Veta walia na nyenzo zilizopitwa na wakati

 


Wanafunzi wa chuo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi (Veta Kihonda) wameeleza kuwa wamekuwa wakifundishiwa na vifaa ambavyo teknolojia iliyopita na wakati.


 Wakizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Afisa tawala wilaya ya Morogoro wamesema vifaa vinavyotumika chuoni hapo kufundishia ni teknolojia ya zamani.


Mwanafunzi wa mwaka wa pili fani ya umeme wa magari, Nestory Pius amemweleza afisa huyo kuwa ni wakati wa serikali kuona umuhimu wa kupeleka vifaa vya kisasa ambavyo vinaendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuendena na kasi ya mabadiliko ya dunia.


Nestory amesema kuwa mabadiliko ya teknolojia yatasaidia chuo hicho kuwa na wahitimu ambao wamepata kwa kufundishwa kozi inayoendena na mabadiliko ya tekonolojia.


“Tunashukuru serikali imeanza kulifanyia kazi kwa kuleta vifaa vipya na kisasa katika karakana mpya ya umeme wa magari na useremala ambapo vifaa hivyo vitasaidia kuongeza ujuzi katika fani.”alisema Nestory katika taarifa ya wanafunzi.


Mkuu wa chuo cha Veta Kihonda Maganga Kashindye alisema chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vya veta ambavyo vinavyosimamia mfumo wa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na vijana wengi kupatiwa mafunzo na kujikwamua na tatizo la ajira kwani wahitimu wengi wanaohitimu wana uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa.


Kashindye ametaja mafunzo hayo kuwa ni ufundi wa majokofu na viyoyozi, ushonaji wa nguo, ufundi wa zana za kilimo, ufundi wa umeme wa magari, ufundi uashi, ufundi magari, ufundi wa umeme wa majumbani, ufundi wa uchongaji vyuma na ufundi seremala.


“Licha ya masomo hayo wanafunzi wamekuwa wakipata masomo ya kiada kama sayansi ya uhandisi, hisabati, michoro ya ufundi, matumizi ya kompyuta na kujifunza kiingereza na mbinu za mawasiliano sasa vijana wakitoka hapa wanakuwa wameiva kwa sababu wanakuwa wamejifunza ujasiriamali na stadi za maisha.”alisema Kashindye.


Afisa tawala wilaya ya Morogoro, Janeth Chata alisema kuwa vyuo vya veta ni sehemu muhimu ya kuwaandaa vijana kukabiliana na soko la ajira na vijana kupata ujuzi wa kujiari wao wenyewe.


Janeth alisema inafaa ieleweke kuwa idadi kubwa ya watu ni ambao ni nguvukazi ya taifa inapungua kwa kushiriki kutokana na magonjwa yanayoodhofisha kinga za mwili hivyo ni vyema sasa kujikinga na magonjwa yanayoweza kuepukika.


“Vijana tunzeni afya ili muweze kulisaidia taifa katika kuchapa kazi lakini kozi mnazosomea na kupata ujuzi muelekeze akili huko na kuachana na kudandia maisha ambayo yatawaharibia mifumo ya maisha.”alisema Janeth.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi