60 wahofiwa kuuawa shule ikishambuliwa na bomu Ukraine


 Makumi ya watu wanahofiwa kufariki dunia baada ya shule moja mashariki mwa Ukraine, kushambuliwa na bomu katika eneo ambalo vikosi vya serikali vinapambana na wanajeshi wa Urusi na watu wanaotaka kujitenga.


Gavana wa mkoa wa Luhansk, Serhiy Gaidai, alithibitisha vifo vya watu wawili, akisema watu 60 wanahofiwa kufa kwa kufunikwa chini ya vifusi vya shule huko Bilohorivka.


Takriban watu 90 walikuwa wamejihifadhi katika jengo hilo ambapo 30 waliokolewa, saba kati yao wakiwa wamejeruhiwa, aliongeza.


Bw Gaidai alisema kuwa ndege ya Urusi ndiyo iliyoshambuliwa majengo ya shule hiyo kwa bomu siku ya Jumamosi.


Madai yake hayakuweza kuthibitishwa kutokana na kutokuwepo kwa majibu ya haraka kutoka kwa Urusi.


Luhansk imeshuhudia mapigano makali huku wanajeshi wa Urusi na wapiganaji wanaotaka kujitenga wakijaribu kuzingira vikosi vya serikali, zaidi ya miezi miwili tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.Tangu uvamizi huo uanze tarehe 24 Februari, Umoja wa Mataifa umerekodi vifo vya raia 2,345 na wengine 2,919 kujeruhiwa nchini Ukraine, huku zaidi ya watu 12milioni wakiikimbia nchi hiyo kuhofia usalama wao.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia