Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Biden kuzifariji familia za wa wahanga wa shambulizi la shuleni Uvalde

 


Rais Joe Biden wa Marekani na mkewe Jill Biden watakwenda mji wa Uvalde katika jimbo la Texas siku ya Jumapili kuzifariji familia na kutoa heshima kwa wahanga wa shambulizi la bunduki shuleni ambapo wanafunzi 19 na walimu wawili waliuawa. 

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre amesema rais Biden atakutana na viongozi wa jamii na kidini na familia za wahanga wa shambulizi hilo la kikatili. 

Mauaji hayo katika shule ya msingi ya Robb yamesababisha mjadala mwingine wa kitaifa juu ya kudhibiti umiliki wa bunduki nchini Marekani. 

Biden kwa mara nyingine ametoa wito wa kuweka taratibu mpya kuhusu ununuaji na umiliki wa bunduki nchini mwake. 

Akifafanua ibara ya katiba ya Marekani inayowapa watu haki kuwa na silaha, Biden amesema haki hiyo pia ina mipaka yake. 

Ameeleza kuwa mtu hawezi kumiliki silaha za aina zote na amesisitiza kwamba wakati wote pamekuwapo na mipaka.


Post a Comment

0 Comments