Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Mtendaji atuhumiwa kumiliki genge la uhalifu,wananchi wataka kuteketeza familia yake


Njombe.

Mtendaji wa kijiji cha Idunda kata ya Yakobi mjini Njombe bwana Otimali Mbangala maarufu kwa jina  la mtendaji wa Tanzania ameibuka kuwa mjadala mzito kwa wananchi wa kijiji jilani cha Nundu kilichopo mji wa Njombe mara baada ya wananchi wa kijiji hicho kudai kuwa anamiliki genge la wahalifu wanaotekeleza wizi katika kijiji chao.


Wananchi wameibua mjadala huo katika mkutano wa kijiji chao uliokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali yakiwemo maswala ya ulinzi na usalama na kudai kuwa mtumishi huyo anayejiita mtendaji wa Tanzania kwa mantiki ya kuweza kufanya kazi mahali popote nchini amekuwa akitetea wezi wanapokamatwa huku baadhi yao wakiwa ni miongoni mwa watu kutoka kwenye familia yake.

"Huu mtandao wa wizi ni mtandao wa mtendaji wa Tanzania hili lazima tuliangalie kwa makini sana kama kuna mtu yuko juu ya sheria sawa,tunapozungumza hili ni kwamba imefika mwisho kwasababu tukio la kwanza mpaka la tatu wezi ni hao hao na walikamatwa lakini hawakuchukuliwa sheria yeyeote na anayefanya kazi ni mtu huyo huyo mtendaji wa Tanzania"wamesema baadahi ya wananchi

Wananchi wa kijiji hicho wamedai kuwa kwa sasa wizi umekithiri pamoja na kuchomewa nyumba katika maeneo yao huku baadahi ya wezi wamekuwa wakikamatwa lakini wanarudi na kuzidi kutetewa na mtendaji huyo,hata hivyo wananchi hao kutokana na kuchoka matukio hayo wamedai kutaka kuiteketeza familia ya mtendaji huyo.

Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi kituo cha Uwemba Ted Moses Kossam aliyefika kutoa elimu katika mkutano huo ametoa wito kwa wananchi kuwa tayari kutoa ushahidi Mahakamani mara baada ya wahalifu kukamatwa katika maeneo yao kwa kuwa wahalifu wamekuwa wakiachwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

 

Post a Comment

0 Comments