Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Takwimu za Stephen Curry, ashinda tuzo ya MVP NBA

Mchezaji nyota wa Golden State Worriors Stephen Curry ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA ukanda wa Magharibi baada ya kuisaidia timu yake kufuzu fainali ya NBA 2022, baada ya kuifunga Dallas Maverick .

Tuzo hii ya MVP aliyoshinda Curry ya ukanda wa Mahgaribi ni mpya inabeba jina la Magic Johnson na ameshinda tuzo hii baada ya kupigiwa kura na jopo la waandishi wa habari 9. 

Curry ameshinda tuzo hii baada ya kukiongoza kikosi cha Worriors kushinda mchezo wa 5 (game 5) alfajiri ya leo kwa ushindi wa alama 120 kwa 110 dhidi ya Dallas Maverick. Kwenye mchezo huu amefunga amefunga alama 15 pasi za kufunga (Assist) 9 na Rebound 3.

Katika michezo ya fainali wastani wa Stephen Curry kupata alama ni 23.8  kwa mchezo pasi za kufunga (Assists) 7.4 na watastan wa rebound ni 6.6 kwenye michezo 5 ya fainali.

 

Post a Comment

0 Comments