Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Viongozi wa Umoja wa Afrika waanza mikutano ya kilele Malabo

 


Viongozi wa Afrika wanakutana leo kwa mikutano miwili ya kilele katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo. 

Takriban wakuu wa nchi 20 pamoja na wafadhili wanahudhuria mkutano wa kwanza na wa kipekee wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kushughulikia mizozo. 

Mikutano hiyo inafanyika wakati bara hilo linakabiliwa na mizozo, ugaidi na mapinduzi ya kijeshi. 

Kulingana na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, Waafrika wapatao milioni 113 wanahitaji misaada kwa haraka mwaka huu, wakiwemo wahamiaji milioni 48, wanaotafuta hifadhi katika mataifa mengine na vilevile wakimbizi wa ndani. 

Mkutano wa pili wa kilele utafanyika kesho Jumamosi ambapo viongozi watajadili masuala ya ugaidi na mabadiliko yasiyo ya kikatiba, wakati ambapo bara la Afrika linakabiliwa na machafuko yanayoendeshwa na makundi ya itikadi kali katika nchi za Libya, Msumbiji, Somalia, kanda ya Sahel, magharibi mwa Ziwa Chad na nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Post a Comment

0 Comments