Ticker

6/recent/ticker-posts

 


WHO: Karibu visa 200 vya homa ya nyani vyaripotiwa katika zaidi ya nchi 20


 Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema karibu matukio 200 ya ugonjwa wa homa ya nyani yameripotiwa katika zaidi ya nchi 20 ambazo kawaida hazijulikani kukumbwa na miripuko ya ugonjwa huo usio wa kawaida. 

WHO hata hivyo imeelezea janga hilo kuwa linaloweza kudhibitiwa na kupendekeza kuundwa hifadhi ya kutosha kwa ajili ya kutolewa kwa usawa chanjo na madawa yaliyopo kwa sasa kote ulimwenguni. 

Shirika hilo la Afya limesema bado kuna maswali mengi ambayo hayana majibu kuhusu jinsi janga hilo lilianza, lakini hakuna ushahidi kuwa mabadiliko yoyote ya kijenetiki katika kirusi hicho ndiyo yaliyosababisha mripuko huu ambao haujawahi kutokea. 

Mapema wiki hii, mshauri mwandamizi wa WHO alisema mripuko wa homa ya nyani barani Ulaya, Marekani, Israel, Australia na kwingineko huenda ulihusishwa na ngono katika matamasha mawili ya starehe yaliyofanyika karibuni nchini Uhispania na Ubelgiji.


Post a Comment

0 Comments