F Wakazi wa Mabwepande waanza kulipia ardhi yao | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wakazi wa Mabwepande waanza kulipia ardhi yao


Zaidi ya wakazi 1800 katika kata ya mabwepande mkoani Dar es salaam wameanza sasa kulipia maeneo yao kwa ajili ya kuandaa hati na kumiliki ardhi mara baada ya kuzinduliwa kwa utoaji wa namba ya namba yaani control sambamba na kutoa barua za utambulisho.


Zoezi la Kuwapatia namba na barua Maalum linatokana na kukamilika kwa Zoezi la Upimaji Ardhikuwa likiendeshwa na Shirika la Maendeleo la DDC mkoa wa Dar es salaam kwa wakazi hao waliopewa ardhi inayomilikiwa na Shirika hilo ambapo baada ya Makubaliano na Serikali ya Mkoa wa Dsm wananchi hao walikubali kulipa. shilingi 6500 kwa Square Mita Moja.


Baadhi ya Wananchi wamelipokea zoezi hilo kwa furaha kwa kuwa na kumaliza kumaliza Migogoro ya Ardhi iliyodumu katika kata ya Mabwepabde kwa zaidi ya miaka 20 lakini pia kupata Umiliki halali wa Ardhi kupitia hati hiyo watakazopata huku wakishukuru serikali kupitisha shirika hilo.

Post a Comment

0 Comments