Kiongozi wa Indonesia anaitaka Marekani kufanya zaidi kukomesha 'ukatili' Gaza

 


Rais wa Indonesia Joko Widodo amemshinikiza mwenzake wa Marekani, Joe Biden, kuchukua hatua zaidi za kuwezesha usitishaji wa mapigano katika mzozo huo.


"Indonesia ilitoa wito kwa Marekani kufanya zjuhudi za kukomesha ukatili Gaza,"


Bw Widodo alisema hayo kufuatia mazungumzo katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu.


"Hili [kusitishwa kwa mapigano] ni lazima kwa ajili ya ubinadamu."


Hapo awali alisema atamletea Biden "ujumbe mzito sana" kutoka kwa mkutano wa kilele wa viongozi wa Waarabu na Waislamu mwishoni mwa juma, ambao ulitaka mapigano yakomeshwe na kuilaani Israeli.


Indonesia ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.


Widodo pia alisema kabla ya mkutano wake na rais wa Marekani kwamba atatoa ujumbe maalum kwa Biden kutoka kwa kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas.


Marekani hadi sasa imekataa wito wa kusitishwa kwa mapigano, ikisema hilo litawawezesha Hamas kujipanga upya na kushambulia tena.


Badala yake, imekuwa ikishinikiza kusitishwa kwa muda mrefu kwa kibinadamu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia