Watoto wachanga na wagonjwa tayari wamefariki

 


Dkt Mohamed Abu Selmia, meneja wa hospitali muhimu ya Al-Shifa mjini Gaza, ameambia BBC kuwa watu 32 wamefariki katika siku za hivi karibuni.


Watoto watatu waliozaliwa kabla ya wakati wao na watu saba walikuwa wamekufa kutokana na ukosefu wa oksijeni, alisema.


Wagonjwa wengine kadhaa wanaohitaji tiba ya figo ya dialysis kwa dharura wanatarajiwa kufariki katika "siku chache zijazo" kwani matibabu hayapatikani tena, alisema.


Hospitali inakaribia kukosa mafuta na rasilimali nyingine ili kuendelea kufanya kazi - huku watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda wakiwa wametolewa nje ya vifaa maalumu vya kuwatunza (incubators) ambavyo havifanyi kazi tena. Kuna zaidi ya wagonjwa 600 waliojeruhiwa pia.


BBC ilimuuliza daktari iwapo jeshi la Israel lilikuwa na mawasiliano yoyote kuhusiana na kuwahamisha wagonjwa au watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.


Israel imesema kuwa imetuma mafuta karibu na hospitali na rasilimali nyingine.


Lakini daktari alisema: “Hapana, hawajafika, badala yake tuliwasiliana não ... lakini mpaka sasa hatujapata majibu.


"Kuna mazungumzo kuhusu kuwahamisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika."


Abu Selmia alisema hospitali hiyo pia imewasiliana na Shirika la Msalaba Mwekundu ili kujaribu kuratibu mazishi ya miili hiyo, ambayo ilikuwa takriban 150 katika hospitali hiyo - lakini iliambiwa kwamba kwa sasa haiwezekani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia