Airtel yatangaza kurejea huduma za intaneti huku ikiendelea kurudisha vifurushi kwa wateja


Kampuni ya simu za mkono ya Airtel Tanzania imetangaza kurejea kwa huduma za intaneti baada ya kutokea kwa hitilafu kwenye mkongo wa mawasiliano wa baraharini (submarine sea cables) mnamo siku ya Jumapili Mei 12 2024 na kusababisha kukosekana kwa huduma za intaneti nchini.

Taarifa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano  wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amethibitisha kuwa huduma za intaneti zimerejea kikamilifu na hivyo wateja wanaweza kuendelea kufurahia kutumia huduma za intaneti kama kawaida.

“Naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia wateja wote wa Airtel kuwa huduma zetu za intaneti zimerejea baada ya hitilafu iliyouathiri mkongo wa mawasiliano baraharini (submarine sea cable) mnamo siku ya Jumapili 12 Mei 2024 na kusababisha kukosekana kwa huduma za intaneti nchini.

Airtel Sisi kama watoa huduma za mawasiliano tunatambua usumbufu ambao wateja wetu wamepata na naomba kuchukua fursa hii kuwaomba radhi kwa tatizo na kuahidi ya kwamba Airtel Tanzania tutaendelea kuhakikisha kutoa huduma zilizo bora na nafuu kwa wateja wetu”. alisema Mmbando.

Mmbando aliongeza kuwa Airtel Tanzania inaendelea kuwafidia wateja wake vifurushi ambavyo hawakuweza kuvitumia kutoka na tatizo hilo.

Airtel Tanzania announces fully restoration of internet services and bundle refund.

 Airtel Tanzania has announced restoration of internet services after services disruption occurred on 12 May 2024, a problem which caused unavailability of internet countrywide.

A Press Release issued today in Dar es Salaam, by Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando has said that internet services have fully been restored and therefore customers can now continue using services as normal.

“Airtel Tanzania takes this opportunity to announce to our esteemed customers that internet services have now fully been restored after disruption occurred on Sunday May 12, 2024, from 11:00hrs due to failure of submarine optic fiber cables which caused unavailability of internet services country wide.

Mmbando added’ ‘Airtel Tanzania is refunding customers who were unable to use their bundles during that period and he promise to continue ensuring a reliable connectivity as usual.

The disruption had been caused by faults in multiple undersea cables, which are vital for connecting systems and companies that support internet and telecommunications infrastructure in the region. The outage affected countries in East Africa, leaving approximately 80 million users without internet.

Post a Comment

0 Comments