Mke wa balozi adai kuvamiwa na kutishwa


MKE wa balozi wa Tanzania anayemaliza muda wake nchini Comoro, Pereira Ame Silima, Mwanaamina Farouk amelalamikia kuvamiwa na kutishiwa maisha nyumbani kwake.

Wakati akidai kuvamia, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba linafuatilia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanaamina alisema matukio ya kuvamiwa yametokea mara mbili huku la hivi karibuni lilitokea Mei 5 mwaka huu saa 8: 00 usiku nyumbani kwake Mazizini.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo tukio la kwanza, nyumbani kwake hakuwa na ulinzi lakini baada ya kutokea aliweka walinzi wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) hivyo waliporejea mara ya pili walifanikiwa kuwadhibiti.

Hata hivyo alidai waliovamia nyumbani kwake hakuna kitu chochote walichochukua wala kuchukuliwa lakini anaishi kwa hofu kutokana na jambo hilo.

“Mara ya kwanza nilikuwa naswali baada ya kumaliza kuswali, nikasikia kishindo baadaye walipoingia ndani nikajificha na wanangu, waliingia chumbani kwangu wakaangali lakini sisi hawakutuona na tulipiga simu polsi wakaja,” alisema

Kwa mujibu wa Mwanaamina watu hao walipanda ukuta kwenye varanda wakapenyeza mkono wakatoa lock na kuingia ndani.

“Kama wamekuja mara ya kwanza wakarudi mara ya pili, sijui wanataka nini na lini kitatokea mimi hapa nina watoto wadogo kwahiyo tunaishi kwa hofu,” alisema na kuongeza

Kama wameshindwa kunipata lakini hawajaiba kitu kwahiyo inawezekana hawataki vitu wanataka mtu, watoto wamekuwa na hofu hawawezi kukaa ndani,”

Alisema baada ya tukio hilo alipiga simu polisi na walikuja kuangalia ila walipoondoka wakasema watarudi kuchukua maelezo lakini hawajarudi na hajui kinachoendelea.

“Kinachotisha zaidi hawakuiba ila wanapekua vitu, kwahiyo hatujui kinachoendelea kama mtu anakuja na silaha anakuja, kwasbabu mwizi wa kawaida angeiba na kuondoka,”

Akizungumza tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi jana, Richard Mchonvu alikiri kupokea taarifa za tukio hilo Mei 4, 2024 saa 8: 00 usiku.

“Askari waliokuwa doria walipokea taarifa kutoka kwenye uongozi wa JKU wakielezwa kwamba huko mazizinikuna eneo wanalinda wakaomba msaada zaidi na walifika,” alisema 

Hata hivyo alisema baada ya askari hao kufika eneo la tukio waliona mazingira yapo salama na hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea kwahiyo wakaendelea na shghuli zao.

“Ni kweli taarifa zilifika kwasababu chombo kinacholinda pale kipo imara, lakini tunaendelea kufuatilia kwa ndani, ila nimombe huyo amma aje ofisini tujadili kuhusu sula la usalama wake, nipo tayari,” alisema Mchonvu

Wakati huohuo Jeshi la polisi mkoa huohuo limeanzisha operesheni maaalumu kukabiliana na matukio ya unyang'anyi yambayo yametajwa na jeshi hilo kuwa tishio kisiwani humo.

kwa mujibu wa Mchomvu, ndani ya miezi sita wamekamata vijana 117 kati ya hao 60 ni matukio ya unyanganyi.

"Kati ya vijana hao, watuhumiwa 60 wamekamatwa na makosa unyang’anyi wa kutumia silaha za jadi (mapanga), unyang’anyi wa kutumia nguvu, shambulio, mauaji na watuhumiwa 57 walikamatwa kwa makosa ya wizi," alisema Mchomvu.

Kadhalika, alisema unyang’anyi huo unafanywa na vijana wanaotumia dawa za kulevya kwa kuanzisha vikundi mitaani vinavyotumika kuwavizia wananchi na kuwanyang’anya mali zao kwa kutumia silaha za jadi.

"Vijana hao wanatembea wakiwa wamebeba mapanga ila wakikamatwa na kuulizwa wanadai ni utamaduni wa Zanzibar mwanaume kutembea akiwa na panga au kisu, amesema halikubaliki kwani hiyo ndio njia wanayoitumia kufanya uhalifu, hili tunataka tulikomeshe," alisema Mchomvu

Post a Comment

0 Comments