Wakamatwa kwa kumteka mtoto Mbeya


Na. Mwandishi, Jeshi la Polisi- Kilimanjaro

Jeshi la Polisi limesema limefanikiwa kumpata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 05
mwanafunzi wa Shule ya awali Isaiah Samartan iliyopo jijin Mbeya aliyeripotiwa kupotea mei
15,2024 muda wa saa 11:45 jioni huku likiwashikilia watuhumiwa watatu kuhusiana na tukio
hilo.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime
amesema tukio hilo liliripotiwa na Baba mzazi wa mtoto aitwaye Layson Mkongwi, Mfakanyakazi wa
Kampuni binafsi huko Jijini Mbeya ambaye alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika na
kumweleza kuwa hatampata mtoto wake hadi atakapomtumia kiasi cha shilingi milioni ishirini
(20,000,000=).

Ameongeza kuwa Jeshi hilo baada ya kupokea taarifa hizo lilianza uchunguzi na kufanikisha
kupatikana kwa mtoto huyo akiwa salama Pamoja na mtuhumiwa ambae ni Winfred Martin
Komba, miaka 36, Mkazi wa Vingunguti Dar es Salaam ambaye ndiye aliyekuwa akimpigia simu
baba mzazi wa mtoto na kumtishia atoe fedha.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Mama mzazi wa huyo mtoto aitwaye Agnes Jacob
Mwalubuli mkazi wa Isyesye Mbeya ambaye alipanga njama na mtuhumiwa ili kujipatia kiasi
hicho cha fedha kutoka kwa Baba mzazi wa mtoto huyo.

Mtuhumiwa Wilfred Komba baada ya kuhojiwa alieleza kuwa baada kupanga njama hizo
alifanikiwa kumchukuwa mtoto huyo Mei 15, 2024 na kwenda kumficha kwa rafiki yake aitwaye
Hamida Gaudence Njuu anayeishi Jijini Mbeya.

Sambamba na hilo amesema Ufuatiliaji ulifanyika na Mei 24, 2024 majira ya saa saba kasoro
usiku (00.45) mtoto huyo alikutwa nyumbani kwa Hamida Gaudence Njuu huko Simike Mbeya.
DCP Misime amesema tukio hilo limechukuwa muda mrefu kutokana na kila ambalo Polisi
walikuwa wanapanga kwa kumshirikisha mama mzazi wa mtoto huyo wakidhani ana uchungu
na mtoto wake lakini yeye alikuwa akimfikishia taarifa mtuhumiwa mwenzake hivyo kumfanya
aendelee kujificha.

Aidha amesema Jeshi hilo linawashikilia Watuhumiwa hao watatu kwa ajili ya kukamilisha
taratibu zingine ili wafikishwe katika vyombo vya Sheria.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wenye tabia kama hizi wafahamu watajificha kwa muda,
iwe wiki, miezi au miaka ambapo alibainishakuwa Jeshi hilo litawakamata

Aidha wafahamu fika vitendo kama hivi vya kula njama, kuteka, na kujiteka ni uhalifu ambao
haulipi kwani mwisho wake kama Mungu ataendelea kukuweka hai lazima utakamatwa na baya
zaidi inaweza kupelekea familia yako kusambaratika

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia