Mbunge wa Jimbo la Lupembe wilayani Njombe Edwirn Swale amewataka wakazi wa Idongela kijiji cha Lole kata ya Ikuna kuwa na imani na serikali yao na kutembea kifua mbele kwa kuwa inaendelea kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma muhimu.
Swalle ameeleza hayo wakati akizungumza na wakazi wa Idongela alipofanya ziara katika kijiji cha Lole wilayani humo.
"Idongela A na B vyote vimeingia kwenye mkataba na mkandarasi atakuja ili mpate umeme,kwa hiyo kwa upande wa kata ya Ikuna kitingoji cha kwanza ni Kitewele kinapata umeme safari hii,kwa hiyo kijiji cha lole peke yenu mpeta vitongoji vitatu"
Swalle amesema "Ninyi mmepata vitongoji viwili lakini kuna wenzenu bado kwa hiyo ndugu zangu hiyo ndio serikali yenu na nimekuja kuwapa mrejesho na mkandarasi atakuja hapa mtapata umeme na mtachaji simu hapa na kusaga unga hapa"
Aidha licha ya kutoa wito huo,Swalle ameweza kuchangia fedha kiasi cha shilingi laki tano ili kusaidia kusogeza mawe kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya msingi Idongela
"Lakini nimeambiwa mna mawe yako porini na itabidi yasombwe kuja hapa na ninawachangia laki tano ili kusogeza mawe kuja hapa shuleni angalau na mie niwe nimetoa mchango wangu"
Amewataka wakazi wa kijiji hicho kuwa na imani kwa kuwa serikali haiwezi kuwaacha kwenye giza na mwaka huu umeme utafika katika vitongoji hivyo.
Nao baadhi ya wakazi wa Idongela akiwemo Juliet Mwinami na Braiton Kipagatye wamepongeza jitihada zinazofanywa na Mbunge kwa kushirikiana na serikali huku wakidai kuwa swala la umeme kwao litakuwa na msaada kuwa katika maendeleo.
"Nipende kukushukuru kwa kuwa umezungumza na endapo umeme utakuja sisi tutakuunga mkono zaidi na umeme umeshagusa kwenye nyumba zetu baadhi"amesema amesema Juliet
0 Comments