Airtel Tanzania imezindua minara miwili mipya ya mawasiliano katika maeneo ya Simanjiro – Lebosoiti na mkoa wa Mara kata ya Mugumu, hatua itakayoboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na intaneti kwa wakazi wa maeneo hayo.
Uwekezaji huu ni sehemu ya mkakati endelevu wa Airtel Tanzania wa kufikisha huduma zake za mawasiliano kote nchini, hususan katika maeneo ambayo hapo awali hayakuwa na huduma za kutosha.
Mnara wa Simanjiro (Lebosoiti) utahudumia vijiji vya jirani ambavyo ni ambuleti na loksale, na kuwawezesha wakazi kupiga simu, kutumia huduma za fedha kwa njia ya simu pamoja na kuunganishwa na intaneti kwa urahisi zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Simanjiro, Paulo Emanuel, alisisitiza umuhimu wa maendeleo hayo kwa wakazi wa eneo hilo. “Uzinduzi wa mnara huu ni hatua muhimu katika kuboresha mawasiliano na upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa wananchi wa Terrat na maeneo ya jirani.
Huduma hii ya mawasiliano itawezesha kukua kwa shughuli za kijamii na upatikanaji wa huduma muhimu,” alisema.
Kwa upande wa Mkoa wa Mara, mnara mpya wa Mugumu utahudumia jamii nne zinazouzunguka mnara huu mpya, na hivyo kuboresha mtandao na ubora wa huduma kwa wakazi wa eneo hilo.
Meneja wa Tawi la Airtel Kanda ya Mara, Bw. Emmanuel John, alisema mnara huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha wananchi na fursa mbalimbali.
“Upanuzi huu wa mtandao utawezesha jamii za Mugumu na maeneo ya jirani kuendelea kuwasiliana, kutumia huduma za kifedha kupitia simu na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali,” alisema.
Akishuhudia tukio la uzinduzi wa mnara huo huko Lebosoit, Afisa Mtendaji wa kijiji,Bw. Hosea Nisolo aliipongeza Airtel Tanzania kwa uwekezaji huo, akieleza kuwa utakuwa na mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya wananchi na maendeleo ya jamii.
“Mnara huu utaimarisha sana mawasiliano katika eneo letu. Wananchi sasa wataweza kupiga simu kwa uhakika, kutumia huduma za simu na kupata intaneti kwa urahisi, hali itakayosaidia shughuli za kibiashara na kuongeza upatikanaji wa taarifa,” alisema Afisa Mtendaji wa kijiji.
Naye mkazi wa Simanjiro kijiji cha Lebosoiti Bw. Lengere Ngisei , Anaelezea furaha ya wanakijiji hao ambao kwa asilimia kubwa wanajishughulisha na Ufugaji na Kilimo “Tumehangaika kwa muda mrefu kupata huduma ya mtandao katika kijiji chetu bila mafanikio lakini leo Airtel mmeamua kutuunganisha sisi na ndugu zetu waliopo mbali kupitia mnara huu mpya mlioujenga” Alisema Lebosoiti
Airtel Tanzania inaendelea kuweka kipaumbele katika upanuzi wa mtandao kama sehemu ya dhamira yake ya kukuza ujumuishaji wa kidijitali, kuhakikisha jamii zote nchini zinapata huduma bora, nafuu na za kuaminika za mawasiliano na intaneti.
Kupitia uwekezaji endelevu wa miundombinu, Airtel inaendelea kuunganisha watu, kuwawezesha jamii na kuchangia maendeleo ya taifa.



0 Maoni