F Chama wa Babati ajinyonga hadi kufa , unywaji wa pombe watajwa kuwa chanzo. | Muungwana BLOG

Chama wa Babati ajinyonga hadi kufa , unywaji wa pombe watajwa kuwa chanzo.


Na John Walter-Babati

Mkazi wa mtaa wa Nangara Kati, mjini Babati, mkoani Manyara, Maulid Shaban (Chama) anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nangara Kati, Bw. Hamad Mungere, tukio hilo lilitokea jana Januari 23 majira ya mchana, ambapo marehemu alijinyonga akiwa nyumbani kwa dada yake.

Mwenyekiti amesema kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na changamoto za afya ya akili zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizochangia tukio hilo la kusikitisha.

Marehemu ameacha watoto watatu, hali iliyoacha huzuni kubwa kwa familia, ndugu na wakazi wa eneo hilo.

Bw. Mungere ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, akisisitiza kuwa vitendo vya kujiumiza au kujiua si suluhisho la changamoto za maisha na havifai kabisa katika jamii.

Amehimiza wananchi kutafuta msaada wa karibu pale wanapokumbana na matatizo ya kisaikolojia au kijamii.

Mwili wa marehemu umezikwa leo katika mtaa wa Nangara Kati, mjini Babati, kwa mujibu wa taratibu za familia na jamii.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni