F Fainali ya Afcon 2025 watakutana Morocco dhidi ya Senegal | Muungwana BLOG

Fainali ya Afcon 2025 watakutana Morocco dhidi ya Senegal


Na John Walter


Baada ya ushindi wa timu ya Taifa ya Morocco dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria kupitia mikwaju ya penati, timu ya Morocco imehakikisha nafasi yake katika fainali ya AFCON 2025 itakayopigwa nchini Morocco.

Morocco itakutana na Senegal, ambayo iliingia fainali baada ya kuifunga Egypt 1-0, bao pekee lililofungwa na Sadio Mané.

Hii ni fainali itakayokuwa ya kuvutia sana, ikikutana vigogo wawili wa soka barani Afrika:
Senegal: Inajivunia safu thabiti ya ulinzi na nguvu ya mashambulizi kutoka kwa nyota kama Sadio Mané.
Morocco: Imethibitisha nguvu yake kwenye ulinzi thabiti na nidhamu ya hali ya juu, huku wakiunda ushindi muhimu dhidi ya Nigeria katika mikwaju ya penati.

Fainali ni Januari 18,2026, hiki ni kibao cha ushindani mkubwa kati ya Afrika Magharibi na Afrika Kati.

Mshindi wa tatu ni Jumamosi Januari 17,2026 Nigeria dhidi ya Misri.

#walterhabariupdate #afcon2025

Chapisha Maoni

0 Maoni