Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametangaza
nafasi kwa vijana wa Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na mafunzo ya jeshi
hilo kwa kijitolea kwa mwaka 2026 huku akionya kuwa nafasi hizo haiuzwi na Vijana,
wazazi na walezi kuwaepuka matapeli watakaojitokeza kuwa wanauza nafasi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani
Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la
Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema utaratibu wa vijana hao kuomba
kujiunga na mafunzo hayo utaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya Bara
na Visiwani.
“Utaratibu wa vijana kuomba hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo
hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako muombaji anaishi
kwa vijana wa Bara na Visiwani” amesema
Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema vijana wenye taaluma za Diploma
in information Technology, Diploma in Business Information System, Diploma in
Computer Science, Diploma in information and Communication and Technology ICT.
Taaluma nyingine ni Diploma in Cyber security and Digital forensics,
Bachelor of science in Computer science, Bachelor of Science Information Technology,
Bachelor of Science in Computer Engineering, Bachelor of Science in Business
Information Technology, Bachelor of Science in Cyber Security and Digital Forensics.
Wengine ni Bachelor of Science in Computer Networks and Information Security
Engineering na vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali watapewa kipaumbele
na wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia mikoa yao.
Amesema Usajili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea
utaanza tarehe 26 mwezi wa kwanza 2026 kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani na vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT
mwezi wa pili tarehe 27 hadi tarehe 04 mwezi wa tatu 2026.
Aidha ameendelea kusisitiza kuwa vijana watakaopata fulsa hiyo kuwa JKT halitoi
ajira, pia wala halihusiki kuwatafutia ajira kwenye asasi, vyombo vya ulinzi na
usalama, mashirika mbalimbali ya serikali na yasiyokuwa ya serikali bali hutoa
mafunzo yatakayowasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza
mikataba na JKT.
Amesema sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo
yanapatikana katika Tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz
, amesema Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana watakaopata fursa hiyo kwenda kujiunga
na vijana wenzao ili kujengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, ukakamavu,
kufundishwa stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na
kulitumikia taifa lao.

0 Maoni