F Misri Waaga Mashindano ya AFCON 2025 baada ya kupigwa na Senegal | Muungwana BLOG

Misri Waaga Mashindano ya AFCON 2025 baada ya kupigwa na Senegal


Na John Walter

Timu ya taifa ya Misri (Mafarao) imeaga michuano ya AFCON 2025 baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Senegal katika mchezo mkali uliochezwa usiku wa jana.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na nyota wa Senegal, Sadio Mané, dakika za lala salama, akitumia shuti kali la mbali lililoshindikana kuzuiwa na kipa wa Misri.

Ushindi huo unaipa Senegal tiketi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano hayo yanayoendelea kufanyika nchini Morocco.

Kwa matokeo hayo, ndoto za Misri kutwaa taji hilo zimefikia tamati mapema, huku mashabiki wao wakibaki na majonzi.

Senegal sasa inasubiri kwa hamu kujua mpinzani wake atakayepatikana kati ya Nigeria au Morocco, timu ambazo zinatarajiwa kuchuana saa tano usiku wa leo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku timu zote zikisaka nafasi ya kukutana na Senegal katika hatua inayofuata ya michuano.
Michuano ya TotalEnergies AFCON 2025 inaendelea kushika kasi, ikishuhudia matokeo ya kusisimua na ushindani mkali kati ya vigogo wa soka barani Afrika. ⚽️

#walterhabariupdate
#SadioMane #scored #in #senegal #vs #Egypt #LiveMatchToday #AfricanCupOfNations #senegalfootball #MatchDay #highlights

Chapisha Maoni

0 Maoni