Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe (CCM) Rebecca Nsemwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bunge Sports Club kwa kupata kura 158 dhidi ya Abbas Tarimba Mbunge wa jimbo la Kinondoni ambaye amepata kura 41 za Wabunge.
Nsemwa ameahidi kukuza michezo nchini kupitia nafasi hiyo aliyochaguliwa na wabunge na kwamba ni matarajio yake kuona wabunge wanafika mbali katika michezo inayoshirikisha Nchi Saba za Afrika Mashariki.
Katima uchaguzi huo Thomas Kampala amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti huku Festo Sanga akichaguliwa kuwa
Meneja wa Timu ambapo majukumu hayo yatatekelezwa kwa pamoja na wajumbe wa kamati tendaji inayoundwa na Saashisha Mafuwe,Zulfa Omar,Agnes Marwa,Chistina Mzava pamoja na Dickson Lutevele.
Bunge Sports Club ni taasisi inayohusika na kukuza michezo na burudani miongoni mwa wabunge na watumishi wa bunge.

0 Maoni