Waziri wa mambo ya
ndani ya nchi, Mathias Chikawe
Chikawe ambaye mwaka 2012 aliangushwa ndani ya chama hicho
alipogombea ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa kutoka wilaya ya Nachingwea.
Mara hii ameangushwa tena katika kinyang'anyiro cha kura za maoni baada ya kuwa
omba ridhaa wanachama hicho ili awe mgombea kwa awamu ya tatu.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo. katibu wa CCM wa wilaya
ya Nachingwea, Leticia Mtimba, alimtangaza Hassan Elias Masala(36) mkuu wa
wilaya Kibondo kuwa mshindi baada ya kujinyakulia kura 6494, aliyefuatiwa na
Chikawe aliyepata kura 5128.
Akiwashukuru wananchi na wanachama waliokwenda katika ofisi
hiyo kusikiliza tangazo hilo
ambao walilazimika kusubiri matokeo hayo toka saa tatu asubuhi hadi saa 11
jioni. Alisema anayodhamira ya kweli ya kweli yakuwahudumia wananchi kama alivyohaidi wakati anajinadi wakati wakampeni.
"Nikibahatika kushinda kwenye uchaguzi mkuu, sitambagua
yeyote bali nitatekeza yale niliyohaidi na ambayo yalinisukuma kuomba ridhaa
yenu wanachama wenzangu" nitashirikiana na kupata ushauri kutoka kwenu
wanachama wenzangu,wananchi,viongozi wenzangu na walionitanguli katika nafasi
ya ubunge iwapo nitachaguliwa katika uchaguzi ujao," alisema Masala.
Wagombea wengine na idadi ya kura za kwenye mabano ni Issa
Mkalinga(469), Amandus Chinguile (1274), Issa Mkalinga(469) Ally Nanjundu(319)
Fadhil Liwaka(1171) Albert Mnali(763) Beno Ng'ittu(797) Mustafa Maliche(427)
Steven Nyoni (1438) Gaston Fransis 671.
Hii ni mara ya pili kwa waziri Chikawe kushindwa uchaguzi,
kwani 2012 aliangushwa katika uchaguzi alipojaribu kutetea nafasi ya ujumbe wa
halmashauri kuu ya taifa wa Chama Cha Mapinduzi mwaka 2012 baada ya kuangushwa
na Fadhili Liwaka(32)