F HISTORIA YA MELI MAARUFU DUNIANI TITANIC ILIYOZAMA MIAKA 100 ILIYOPITA? | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

HISTORIA YA MELI MAARUFU DUNIANI TITANIC ILIYOZAMA MIAKA 100 ILIYOPITA?


WASIFU WA MELI YA TITANIC

RMS Titanic ilikuwa meli kubwa ya abiria ya Uingereza ambayo ilizama katika kina bahari cha Kaskazini mwa Bahari ya Atlantic mwaka 1912 tarehe 15 mwezi machi.

Meli hiyo kubwa sana ilizama wakati ilipogonga mwaba-bahari (Iceberg)wakati ikisafirisha abiria kutoka eneo la Southampton, nchini Uingereza ikielekea nchini Marekani katika jiji la New York.

Meli hiyo ilipozama jumla ya abiria 1,502 walipoteza maisha katika ajali iliyorekodiwa katika vitabu vya historia vya Uingereza kama ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea baharini katika wakati wa amani.
Meli hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni ya White Star Line, wakati ikizama ilikuwa ndiyo meli kubwa zaidi duniani.

Mjenzi wa meli hiyo ilikuwa ni kampuni ya Harland and Wolff shipyard ya Belfast.
Wakati ikizama TITANIC ilikuwa imebeba abiria jumla ya 2,224 pamoja na wafanyakazi wa meli.
Kwa mujibu wa Historia meli hiyo wakati ikizama ilikuwa imewabeba baadhi ya matajiri wakubwa wa dunia kwa wakati huo lakini pia watu wa kawaida kama vile wahamiaji waliokuwa wakihama Uingereza yaani Great Britain ,Ireland na Scandinavia kwenda Amerika ya Kaskazini kutafuta maisha.

Meli hiyo iliundwa kama meli kubwa ya starehe ambapo ndani ilikuwa na mabwawa ya kuogelea maarufu kwa kiingereza kama Swimming Pool ,Maktaba,Hotel za hadhi ya juu,na Kibini za gharama kwa ajili ya abiria wenye uwezo mkubwa sana wa kifedha.

Pamoja na kutengenezwa katika muundo wa kisasa kwa wakati huo ambao ungewezesha kupatikana kwa msaada wakati wa ajali bado meli hiyo ya kifahari haikuwa na meli ndogo za kutosha kukidhi mahitaji ya kuokoa watu wote ambao wangepata ajali kama ilivyotokea.

Wakati inazama ilikuwa na meli ndogo chache ambazo zilisaidia kuokoa maisha ya abiria 1,178 tu.
Mara baada ya kuondoka Southampton mnamo tarehe 10 Aprili 1912, Titanic ilitia nanga Cherbourg nchini Ufaransa na Queenstown (leo Cobh) huko Ireland kabla ya kuendelea na safari.

Ajali yenyewe ilitokea mnamo tarehe 14 Aprili 1912, kiasi cha maili 375 (sawa na km 600) Kusini mwa Newfoundland, mara baada ya meli hiyo kugonga mwamba muda wa saa tano na dakika 40 usiku.

Mara baada ya kugonga mwamba huo sehemu ya omo ya meli ilipasuka na hatimaye kuruhusu maji kuingia ndani katika vyumba vya chini vya meli hiyo hali iliyosababisha meli kuanza kuelemewa na hatimaye kuanza kuzama.

Wengi wa Abiria waliosalia katika meli hiyo walikufa mara moja kutokana na mkondo bahari wenye baridi kali na walikufa kwa hypothermia.

Abiria wengi waliokuwa katika vyumba vya meli vya daraja la pili inaelezwa walikufa kutokana na Mabaharia kutekeleza sera ya Okoa Watoto na Wanawake Kwanza’’.

Saa mbili baada ya meli ya Titanic kuzama Meli ya uokozi Cunard liner RMS Carpathia iliwasili 
katika eneo la ajali ambapo ilifanikiwa kuwaokoa manusura 705.

Ajali hiyo ambayo ililalamikiwa kwa uzembe wa vyombo vya kudhibit usalama wa baharini ilisababisha kuboreshwa kwa sheria zinazolinda usalama wa safari za baharini huko nchini Uingereza na Marekani.

Miongoni mwa hatua hizo ni ile ya kuanzishwa kwa sheria ya usalama baharini ya mwaka 1914 inayojulikana kama International Convention for the Safety of Life at Sea (SOLAS), ambayo bado inatumiwa hadi hivi leo

Katika ajali hiyo wengi wa wahanga wa ajali walipoteza mali zao zikiwemo fedha lakini wengine walipoteza ndugu na jamaa zao hususani jamaa ya wafanyakazi wa meli hiyo wa Southampton,abiria walionusurika wengi wao walisaidiwa na mashirika ya misaada na michango iliyotolewa na serikali.
Hata hivyo masalia ya Meli hiyo bado yamo ndani ya Bahari ya Atlantiki hadi hivi leo kina cha Futi 12,415 (sawa na Mita 3,784).

Masalia ya Meli hiyo yaligunduliwa mwaka 1985, ambapo wataalamu wa masuala ya historia wamekuwa wakichukua vitu mbalimbali kutoka kwenye meli hiyo na kuviweka katika Makumbusho ya Taifa ya nchi mbalimbali duniani zikiwemo Uingereza na Marekani.

Titanic bado inabaki kuwa Meli maarufu iliyopata kujengwa duniani katika zama za ‘historia Mpya’ na imeandikwa katika machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu .