Aliko Dangote alizaliwa Nigeria mwaka
1957,april,10.Historia ya utajiri katika familia yake ilianzia kwa babu yake
ambae alikuwa na mashamba makubwa ya peanut ambazo zilikuwa zikisafirishwa
kwenda ulaya na kufanikiwa kupata utajiri mkubwa.
Moyo wa kijasiliamali ulikuwa ndani ya damu ya Dangote kwani
akiwa shule alianza kufanya biashara ya mishumaa.Baada ya kupata shahada yake
katika chuo cha Al- azhar huko Misri ambayo ilikuwa ni shahada ya
biashara,alianzisha kampuni yake ya kwanza ambayo iliitwa DANGOTE GROUP ambayo
ilihusika na biashara ya Cement.Kwa wakati huo tayari familia yake ilikuwa na
uhusiano mzuri na serikali na kwa hivyo ilikuwa rahisi kwake kupata leseni bila
matatizo.Swala la kupata leseni Nigeria ni gumu sana.
Baada ya hapo Dangote alifanya biashara katika nchi
mbalimbali kama Brazil,Amerika
ya Kusini ambako alipata mafanikio makubwa sana
ya kibiashara.Aliweza kuwa na rasilimali nyingi sana
ikiwemo nyumba aliyokuwa ameijenga huko Atlanta.Hata hivyo aliamua kurudi Nigeria na kuirudisha biashara yake Nigeria ili
kukuza uchumi wa nchi hiyo.
Aliporudi Nigeria
miaka ya 90 Dangote alikisaidia chama cha PEOPLES DEMOCRATIC PARTY na
kiliposhinda alifanikiwa kuishawishi serikali kumruhusu kujenga moja kati ya
viwanda vikubwa kabisa vya cement nchini Nigeria.Kwa sasa Dangote ana
wafanyakazi zaidi ya elfu ishirini na tano(25000) na anafanya biashara katika
nchi kumi na nne Afrika nzima.
Mafanikio ya Dangote ni mengi kiasi kwamba unaweza kujaza
vitabu kadhaa lakini kwa kifupi anafanya biashara nyingine kama chumvi,unga wa
ngano,cocoa,sukari nk.Ana nguvu kiasi kwamba ni rafiki mkubwa na tajiri namba
moja duniani bwana Bill gate na anapoongea Gate humsikiliza.
Hongera mr Dangote na hongera kwa baadhi ya watanzania kama
Rostam Aziz,Mengi,MO pamoja na Bakhresa kwa kuingia katika orodha ya matajiri
Afrika na duniani kwa ujumla na kutuonesha njia.Pia hii inatukumbusha kuwa nchi
zetu za kiafrika sio maskini bali sisi ndio wavivu wa kufikiri na kuzifuata
fulsa.
