JE WAJUA; Ujerumani Iliua Wagonjwa na Walemavu.
Wakati wa utawala wa Nazi chini ya Adolf Hitler, ujerumani
ilianzisha sera ya kuua watu wote ambao walionekana ni dhaifu.
Katika sera hii inasemekana watu zaidi ya laki mbili
waliuawa kati ya mwaka 1940 mpaka mwaka 1945.
Waliouawa walikuwa ni wagonjwa wasiopona na walemavu.
Madaktari walitumika katika zoezi hili.
Tukio hili pia limewahi kutokea nchini Uganda ambapo
mtawala wa kipindi hiko Idd Amin alishutumiwa kukusanya walemavu na kwenda
kuwatupa kwenye mto.
