Mke wa marehemu akilia kwa uchungu.
Akizungumza na waandishi wetu nyumbani kwake, Keko jijini Dar wiki iliyopita, Salome alisema yeye ni mke halali wa Mhingo kwani walifunga ndoa mwaka 2013 na walikuwa wakiishi pamoja Mbagala Kuu.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiandaliwa kwa ajili ya kuagwa.
Salome ambaye alikuwa akizungumza huku muda mwingi akilia, alisema:
“Nilikuwa nimekaribia kujifungua ndiyo maana ndugu zake walimchukua. Muda wangu ulipofika nilikwenda Hospitali ya Mico Mbagala, Dar kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki dunia.
“Sikuwa na nguvu ya kufanya kazi yoyote hali iliyonilazimu kwenda kupumzika nyumbani kwetu, Moshi (Kilimanjaro) kwani kipindi chote hicho hadi kujifungua hakuna aliyekuja kuniona upande wa mume wangu.
Mwi wa marehemu ukiagwa.
“Mume wangu pia alichukia kitendo cha mimi kukatazwa kuongea naye lakini hakuwa na nguvu ya kutoa amri. Niliondoka na kurudi kwangu Mbagala Kuu.
“Kabla mume wangu hajafariki dunia, alikuja shemeji yangu mmoja akaniambia nihame hapa nyumbani akidai wanataka kuipangisha hii nyumba ili wapate fedha za kumtibu mume wangu.
Nilijisikia vibaya, ni ndugu wachache tu wa upande wa mume wangu ndiyo waliokuwa wananipenda.
“Siku hiyo niliamua kwenda kumjulia hali mume wangu na kumuuliza pa kwenda kuishi.
Niliwasalimia ndugu waliokuwepo lakini hakuna aliyeniitikia. Wakanikataza kuongea na mpendwa wangu. Nikaenda kutoa taarifa kwa uongozi wa Kanisa Katoliki Mbagala Kuu, walishangazwa na kitendo hicho.
“Tukafuatana na baadhi yao na wasimamizi wa ndoa yetu hadi alipo mume wangu. Walipouliza, walijibiwa kuwa mimi nilimtelekeza ndugu yao. Basi tukaondoka maana hakukuwa na maelewano mazuri.
Wakiaga kwa simanzi.
Ijumaa iliyopita, Salome alifuatana na ndugu zake kwenda kumzika mumewe (akiwa na waandishi wa habari hii). Walipofika, waliambiwa wakae mbali na waombolezaji wengine, wasubiri kuaga na kuondoka ambapo walifanya hivyo.
NDUGU WA MAREHEMU WANAJIBU
Baada ya kusikia maelezo hayo ya upande wa kwanza, waandishi wetu walimtafuta kaka wa marehemu aitwaye Andrew Cosmas ambapo alipoulizwa, alikiri kutokea kwa tukio la mwanamke huyo kutimuliwa kwenye msiba wa mumewe.
Marehemu Boniphace enzi za uhai wake.
Hata hivyo, mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, Cosmas hakupiga simu kama alivyoahidi na hata alipopigiwa tena na mwandishi wetu, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.





