ZAIDI ya kaya masikini 8,000 kutoka vijiji 82 vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa mkoani Iringa zimepata malipo ya nne ya shilingi bilioni 1.2 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kama sehemu ya kuzijengea uwezo wa kiuchumi kaya hizo kwa lengo la kupambana na tatizo la umasikini wa kipato katika ngazi ya kaya.
Fedha ni sehemu ya malipo kwa kaya hizo tangu mpango huo uanze mwezi Julai mwaka jana.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukamilisha malipo hayo katika kijiji cha Maperamengi kata ya Migori katika wilaya ya Iringa, Mratibu wa TASAF wa wilaya hiyo, Bw. Christopher Kajange amesema mpango huo umekuwa msaada mkubwa wananchi hasa waishio vijijini kwani mpaka sasa umesaidia wananchi 1198 ambayo ni sawa na asilimia 14 ya walengwa wote 8431 kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani humo kauli inayoungwa mkono na Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Migori, Bw. Khamis Sabuni ambapo amesema mpango umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makali ya umasikini.