Hivi punde majira ya saa 9:27 asubuhi eneo la Legeza wilayani Newala Barabara ya kuelekea mkoani Mtwara. imetokea ajali imehusisha gari aina ya Subaru-impreza yenye namba ya usajili T684DHY iliyokuwa ikitokea Newala mjini ndipo dereva alipofika katika kijiji hicho (legeza) alishindwa kuimudu gari hiyo hatimaye kuvamia tuta lililokuwa pembezoni mwa barabara kitendo kilichofanya gari hiyo kugeuka mara tatu.Hata hivyo hakuna kifo kilichojitokeza isipokuwa watoto wawili na dereva ni majeruhi,wote walikuwa kwenye gari hiyo na wamepelekwa hospitali ya wilaya ya Newala kwa matibabu zaidi.
Picha za Ajali hiyo..



